August 27, 2017



Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola amesema wanautambua ubora wa Yanga kwamba ni timu bora, lakini wanachotaka ni ushindi.

Matola aliyewahi kuwa nahodha wa Simba, amesema watakachofanya ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara baada ya kurejea ni kuifunga Yanga.

“Ukishinda mchezo wa kwanza unatengeneza mwendo mzuri wa mbele kwa kuwa wachezaji wataanza kujiamini na kufanya vizuri.

“Tunajua Yanga ni timu bora lakini sisi tunataka kufanya vizuri. Hivyo tutajituma na kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema.


Lipuli imerejea Ligi Kuu Bara baada ya kupotea kwa zaidi ya miaka 10 na mechi yao ya kwanza ni dhidi ya mabingwa hao watetezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic