Simba imeshinda mechi yake ya pili ya kirafiki kati ya nne baada ya kuishinda Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Bao la Simba katika mechi hiyo ya ushindani lilifungwa na Emmanuel Okwi.
Pamoja na ushindi huo wa Simba, Mtibwa Sugar walionyesha uwezo mkubwa katika kulisakata soka.
Hiyo inakuwa mechi ya nne ya kirafiki ya Simba kujiandaa na msimu mpya baada ya kuanza kwa kipigo kutoka kwa Orlando Pirates iliyoilaza kwa bao 1-0.
Mechi iliyofuata Simba ikiwa bado Afrika Kusini ilicheza na Bidvest na kutoka kwa sare ya bao 1-1.
Baada ya kurejea nchini, Simba ilicheza dhidi ya Rayin Sports ya Rwanda….na kupata ushindi wa bao 1-0 kabla ya kushinda tena leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment