August 8, 2017


Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sports katika mechi safi ya kuvutia ilivyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ni katika tamasha la Simba Day ambalo hufanyika kila Agosti 8 kusherekea siku maalum ya klabu hiyo.


Bao pekee la mchezo huo, lilifungwa na Mo Ibrahim katika dakika ya 15 baada ya kupokea pasi nzuri ya Emmanuel Okwi aliyeingia kwa kasi katika eneo la hatari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV