August 23, 2017




 Vijana wawili wanaotokea kwenye Kituo cha Soka cha Magnet Youth Sports Organisation cha jijini Dar es Salaam, Daud Damas Maurisi na Malimi Majaliwa Mbasa, jana usiku walikwea pia na kwenda kufanya majaribio katika timu ya vijana ya Machester City.

Daud ambaye ni mlinda mlango na Malimi anayecheza nafasi ya ushambuliaji, wameondoka pamoja na kocha wao, Juma Maulid Maswanya na mmoja wa wazazi wa watoto hao, Majaliwa Majaliwa Mbasa.



Kabla ya kuondoka, vijana hao walikutana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe ambaye aliwaasa kuitumia vema nafasi hiyo ikiwezekana kusajiliwa moja kwa moja na timu hiyo.

“Mnachotakiwa ni kwenda kuitendea haki nafasi mliyoipata, kufanya kwenu vizuri na kujiunga na Manchester City itawafanya vijana wengine kuwa na hamu ya kufuata nyayo zenu,” alisema Mwakyembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic