August 25, 2017



Kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema mechi yao dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii, imemfanya aamini Ligi Kuu Bara haitakuwa lelemama.

Tshishimbi aliichezea Yanga katika mechi iliyoisha kwa Yanga kupoteza kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare ya bila bao ndani ya dakika 90.


“Mchezo ulikuwa mzuri, nimefurahi na kila upande umefanya vizuri, lakini tumefikia hatua ya penalti ambayo timu yoyote inaweza kushinda, kwa upande wangu mchezo huu ndiyo wa kwanza kucheza hapa Tanzania na inaonyesha ligi itakuwa ngumu nimejifunza mengi lakini najiandaa kwa ajili ya ligi ili niweze kufanya vizuri,” alisema Tshishimbi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic