London,
England
KOCHA wa
Arsenal, Arsene Wenger, amewaambia wanaomtaka mshambuliaji wa timu hiyo,
Olivier Giroud kuwa hauzwi.
Arsenal wamekuwa
wakitajwa mara kwa mara kuwa wanaweza kumuuza mshambuliaji huyo raia wa
Ufaransa, lakini kocha huyo amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kuuzwa kwa sasa.
Klabu ya
Everton, imetenga kitita cha pauni milioni 20 zaidi ya shilingi bilioni 50, kwa
ajili ya mshambuliaji huyo ambaye aliifungia Arsenal bao la ushindi kwenye
matokeo ya 4-3 waliyoyapata dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wa ufunguzi
wa ligi wikiendi iliyopita.
“Ni vigumu
kumfanya kila mshambuliaji awe na furaha klabuni kwako, lakini tuna michuano
mingi na naamini kila mmoja anaweza kupata nafasi ya kucheza.
“Nampenda mshambuliaji wangu, Olvier Giroud,
amesema hataki kuondoka nami nafurahi sana kusikia hivyo.
“Nilikuwa nimefungua mlango kwake kwa kuwa
nilijua kuwa ninawashambuliaji wengi lakini amesema hataki kuondoka nami
nimefurahia jambo hilo, hivyo ni vizuri ieleweke kuwa hauzwi,” alisema Wenger.
0 COMMENTS:
Post a Comment