Madrid,
Hispania
KOCHA wa
Real Madrid, Zinedine Zidane, amesema anafuraha kubwa kusaini mkataba wa
kuendelea kuifundisha timu hiyo, lakini haimaanishi kuwa atakaa hapo kwa muda
mrefu.
Zidane
ambaye amekuwa na mafanikio makubwa sana kwenye timu hiyo akiwa ameshatwaa
ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, amesaini mkataba wa
miaka mitatu na timu hiyo.
Baada ya
kusaini, kocha huyo raia wa Ufaransa amesema urefu wa mkataba huo hauna maana
yoyote kama timu hiyo itakuwa haifanyi vizuri uwanjani, inamaanisha kuwa
ataondoka hapo.
“Habari
yangu na Real Madrid ni kubwa kuliko inavyofikiriwa, lakini hapa pana historia
pana kuliko kusaini mkataba na timu hii.
“Nafurahia
kusaini mkataba na klabu hii, lakini haimaanishi kuwa nitakuwa hapa kwa kipindi
chote cha miaka mitatu.
“Nafahamu
hapa nilipo, unaweza kusaini mkataba wa miaka kumi au 20, lakini usikae hapo
zaidi ya mwaka mmoja. Kama sitafanikiwa nitaondoka hapa na Madrid hawawezi
kulalamika,” alisema Zidane.
Zidane
alikabidhiwa timu hiyo mwaka 2016, baada ya kuondoka aliyekuwa kocha wa timu
hiyo Rafael Benitez na tayari ameshatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara
mbili na La Liga mara moja.
Pia
ameiwezesha Madrid kutwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia mara moja na Kombe la
Uefa Super Cup, alipowafunga Manchester United mabao 2-1 wiki iliyopita.
Super payer, super coach... Kazi kwetu watz. Ninmwndo wa makinikia mpaka kwenye soka...
ReplyDelete