September 17, 2017


Gareth Barry amefikia idadi ya mechi za Ligi Kuu England alizocheza gwiji wa Manchester United, Ryan Giggs.

Barry anayekipiga Wes Brom amecheza mechi ya 632 wakati timu yake ikiivaa West Ham katika mechi ya Ligi Kuu England na kufikisha idadi hiyo.

Wakati anacheza mechi hiyo, amemfikia Giggs katika mechi lakini anakuwa mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi na kuanza mara nyingi zaidi.

Giggs mwenye mechi 632 lakini ameanza mechi 522 na Barry ameanza mechi 600 katika kikosi cha kwanza.


Kwa upande wa dakika, Giggs ambaye tayari amestaafu amecheza dakika 46,433 na Barry kacheza dakika 52,781.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic