September 27, 2017



Azam FC wametamba licha ya kuwa ugenini lakini wana nafasi ya kushinda mechi yao ya  ugenini dhidi ya Singida United.

Singida United, itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Jumamosi.

Nahodha wa Azam FC, Himid Mao amesema wamejiandaa vizuri na pamoja na kuiheshimu Singida United. Wamejipanga kubeba pointi tatu katika kila mchezo.

"Sisi tunataka kushinda kila mechi, tunataka pointi tatu ili kujiweka vizuri," alisema.

"Tunajua Singida ni timu nzuri ingawa hatujawahi kucheza nao lakini muhimu kwetu ni pointi tatu," alisema.

Tayari Azam FC imetua mjini Dodoma kwa maandalizi ya mwisho ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya kikosi kinachonolewa na Kocha wa zamani wa Yanga, Hand van der Pluijm. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic