September 29, 2017


Kutokana na kuwa na hofu ya bomu wachezaji wa Tottenham Hotspur walilazimika kuacha mazoezi na kuondolewa eneo la uwanja wao eneo la  Enfield jijini London.

Kulikuwa na hofu ya bomu lililotumika katika vita ya pili ya dunia kuwa katika eneo hilo.

Askari wanaohusika na utaalamu wa mabomu waliitwa katika eneo hilo.

Baadhi ya majirani katika eneo hilo pia waliondolewa na baadhi ya barabara zilifungwa leo asubuhi.


Lakini kufikia saa 4:30 asubuhi, tayari askari hao wataalamu wa mabomu waligundua hakuna hatari.

Baada ya hapo, watu walipewa nafasi ya kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic