September 29, 2017



Hali si nzuri kwa Kagera Sugar kwa kuwa wamekuwa wakienda kwa mwendo wa kusuasua.

Kwani baada ya kupoteza michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara na kutoa sare mchezo moja, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa timu yao hiyo ina matatizo binafsi ambayo hawawezi kuyaweka wazi na kudai kuwa wanapambana na hali yao.

Msimu uliopita Maxime alifanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora kufuatia kufanikisha timu yake kumaliza ligi katika nafasi ya tatu huku ubingwa ukichukuliwa na Yanga.

Kagera Sugar kwa sasa inashikilia mkia kufuatia kuwa na pointi moja hadi sasa ikiwa imepoteza michezo mitatu na kutoa sare mchezo mmoja.

Maxime amesema kuwa, kikosi chake kina matatizo ambayo atayafanyia kazi na si vyema kuyaweka wazi, hivyo anajipanga kuhakikisha wanafanya vyema kwa kutetea nafasi yake ya tatu aliyotwaa msimu uliopita.

“Mwenendo wa timu yetu ni mbaya, lakini kuhusu matatizo katika timu yapo mengi na tunahitaji kufanyia kazi na siwezi kuyaweka wazi kwenye midia, tutapambana wenyewe na kufanyia kazi yote yaliyojitokeza.

“Hatuna madai ya kimaslahi isipokuwa tuna mambo mengine yanayoihusu timu,” alisema Maxime.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic