Kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, inaendelea leo na tokea saa 3:40 hadi sasa, bado yuko kizimbani akitoa ushahidi.
Leo Jumatatu ilikuwa ni siku rasmi kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupokea utetezi wake pamoja na mashahidi wake kuhusiana na tuhuma hizo.
Manji anakabiliwa na kesi hiyo ambayo ilishindwa kusikilizwa Septemba 18, mwaka huu kufuatia wakili wa serikali, Timony Vitalis kumueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa, kesi hiyo iliitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini yeye alidai kuwa alikuwa na safari siku hiyo, hivyo ukianza kutolewa ushahidi atakuwa amechelewa.
Kutokana na wakili wa serikali kueleza hivyo, Hakimu Mkeha alimlaumu Manji kwa kuwa alichelewa kufika mahakamani hapo kabla ya kuomba msamaha huku wakili wake Hajra Mungula akiomba Mahakama iwape kibali cha kupeleka mashahidi wao pamoja na kusikilizwa kwa mfululizo.
Hata hivyo, hakimu Mkeha alikubali maombi yao ya kusikilizwa kesi hiyo mfululizo kwa siku ya leo Jumatatu na kesho Jumanne katika mahakama hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment