September 16, 2017


Mashabiki wa soka mjini Songea wametia fora baada ya kufika kwenye Uwanja wa Majimaji saa 2 asubuhi.

Mashabiki hao wamefika uwanjani hapo mapema wakitaka kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Majimaji dhidi ya Yanga.

Hata hivyo, mashabiki hao hawakuweza kuingia mapema kwa kuwa utaratibu unaonyesha kuazia saa 5 asubuhi hadi 6 mchana ndiyo uwanja unatakiwa kuwa wazi.

Pamoja na kuzuiwa, walionyesha ni wenye subira, wakaamua kusubiri hadi muda ulipowadia wakiwa kwenye foleni na kuanza kuingia.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic