September 5, 2017


BENCHI la ufundi la Simba limeeleza kuwa linahitaji kukaa na mshambuliaji wake wa kimataifa Laudit Mavugo raia wa Burundi kwa lengo la kumpa somo kutokana na kuvurunda katika mchezo dhidi ya Hard Rock ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kumuandaa kisaikolijia.

Mavugo amekumbwa na kadhia ya kuzomewa uwanjani wakati timu yake ilipokumbana na Hard Rock ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa dhidi ya Azam FC uliochezwa wikiendi iliyopita kutokana na kukosa mabao mengi ya wazi.

Akizungumza Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kuwa, Mavugo ni mmoja wa wachezaji wazuri wanaowategemea ndani ya kikosi hicho na kudai kuwa kinachotokea ni mambo ya mpira hivyi wanahitaji kukaa naye kwa ajili ya kumjenga ikiwa ni pamoja a kumuandaa kisaikolijia ili aweze kuwa fiti zaidi.

“Tumefurahi kuona tumefanikiwa kushinda huu mchezo ambao tumeutumia kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Azam FC tutakaocheza nao Jumamosi, tunahitaji ushindi katika mchezo huo.


“Kuhusu mchezaji wetu Mavugo tunahitaji kukaa naye ili tuweze kumuelekeza nini cha kufanya na kumuweka sawa kisaikolojia kwani ni mchezazji mzuri na ana uwezo wa kufunga ambapo anahitaji kupewa maelekezo machache tu kwa ajili ya kumuweka sawa, hivyo tukikaa naye atakuwa vizuri,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic