September 12, 2017


Wakati Manchester United ikitarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa msimu huu, leo Jumanne, kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho amethibitisha kuwa hakutakuwa na mfumo wa kupokezana makipa kama ilivyokuwa msimu uliopita. 

Mourinho amethibitisha kuwa  David de Gea ndiye ambaye ataanza katika kikosi cha kwanza cha timu yake dhidi ya Basle. 

Msimu uliopita, asilimia kubwa ya michezo ya Ulaya kipa aliyetumika kikosini hapo alikuwa ni Sergio Romero lakini safari hii Mourinho ameonyesha kuwa hana mpango huo.

Amesema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwa kuwa De Gea yupo vizuri kwa sasa na hapendi kuwapangia makipa michuano ya kucheza. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic