September 2, 2017



Muda mfupi baada ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), kusema straika wa Yanga, Obrey Chirwa, hana hatia na yupo huru
kuitumikia timu yake, mchezaji huyo amezipiga mkwara timu pinzani.

Juzi Alhamisi, kamati hiyo ilisema Chirwa na Deus Kaseke ambaye
alikuwa Yanga kabla ya kwenda Singida United, hawana hatia baada ya
hapo awali kutuhumiwa kumwangusha mwamuzi, Charles Ludovic.

Wawili hao walituhumiwa kutenda kosa hilo katika mechi yao ya mwisho
ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza ambapo Yanga ilifungwa bao 1-0.

Msuva pekee ndiye aliyekutwa na hatia na amepewa onyo kali. Hata
hivyo, kwa sasa Msuva anaichezea Difaa Al Jadida ya Morocco.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Chirwa alisema: “Hata kama
ningefungiwa kucheza mechi kadhaa za ligi kuu, naamini wachezaji
waliopo wangepambana na kuipa matokeo mazuri timu yangu.

“Kwa sasa mimi bado ni majeruhi, lakini siku si nyingi nitarudi
uwanjani kuendeleza mapambano waliyoyaanzisha wenzangu katika kutetea
ubingwa wetu wa msimu uliopita.

“Nikirudi uwanjani mashabiki wategemee kuuona moto wangu ule wa siku
zote na sasa nitapambana sana kuhakikisha timu yangu inatetea ubingwa
kwa mara nyingine kwani tuna kikosi kizuri na cha ushindani,” alisema
Chirwa.

Chirwa ambaye anasumbuliwa na goti, msimu uliopita alifunga mabao 12
katika Ligi Kuu Bara huku akiibuka Mfungaji Bora wa Kombe la FA akiwa
amefunga mabao sita.


SOURCE: CHAMPIONI (TAYARI LIKO MTAANI)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic