September 6, 2017

KAMPUNI ya kubashiri matokeo ya SportPesa imekabidhi tuzo kwa Gazeti la Championi kutoka Kampuni ya Global Publishers kutokana na ushirikiano mzuri ambao wamekuwa nao.

Wahariri wa Championi wakijadili jambo na viongozi wa SportPesa kuhusu Gazeti la Championi Jumatano lililopo mtaani leo.

 SportPesa imeikabidhi tuzo hiyo leo Jumatano ikiwa ni sehemu ya kushukuru kutokana na ushirikiano mzuri ambao Global kupitia Gazeti la Championi ilionyesha kwa kampuni hiyo mara baada ya timu ya Everton kutua hapa nchini Julai, mwaka huu.

“Tunashukuru kwa ushirikiano wenu kuanzia tulipoanza kufanya kazi nanyi, lakini pia mlituonyesha ushirikiano mzuri sana wakati timu ya Everton ilipotua hapa nchini kucheza na Gor Mahia,” alisema Meneja Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya.












0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic