October 31, 2017



Yanga inatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam keshokutwa kwenda mjini Singida kwa kazi ya kuhakikisha inabeba pointi tatu za Kocha Hans van der Pluijm.

Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga ndiye anayeinoa Singida United ambayo iko katika nafasi ya sita ya Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 13.

Iwapo Singida itashinda dhidi ya Yanga maana yake itakwua imefikisha pointi 16 sawa na Yanga.

Lakini Yanga ikishinda itafikisha pointi 16 na kuendelea kupambana vita ya kukaa kileleni dhidi ya Simba, Mtibwa Sugar na Azam FC.

Singida United itakuwa inauzindua Uwanja wa Namfua mjini Singida ikiwa ni mara ya kwanza ikiuchezea katika mechi ya Ligi Kuu Bara. 

Kabla Singida United walikuwa wakiutumia Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kama uwanja wa nyumbani wakati matengenezo yakiendelea Namfua.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic