October 19, 2017


Kocha msaidizi mpya wa Simba, Masoud Juma amesema anapenda changamoto mpya lakini si mwoga kufukuzwa.

Ikiwa ndiyo siku yake ya kwanza akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari, Juma amesema angependa kufanya kazi ili pate mafanikio lakini ikishindikana, si mwoga kufukuzwa.

“Hata begi langu sijalifunga lote, ikitokea imeshindikana basi nafunga naondoka.

"Kazi ya ukocha ndivyo ilivyo, hautakiwi kuwa na hofu. Lakini nitajitahidi kushirikiana na wenzangu kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema ambaye atakuwa chini ya Mcameroon, Joseph Omog.

Kocha huyo ndiye anachukua nafasi ya kocha msaidizi, Jackson Mayanja ambaye Simba imemtema kutoka katika benchi lake la ufundi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic