October 24, 2017



Unaweza kusema sasa ni uhakika kuwa Kocha Masoud Juma Irambona atakuwa katika benchi la Simba Jumamosi. Lakini itakuwa ni siku ya kwanza katika benchi la moto kwa kuwa linaikutanisha Simba na mtani wake Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru.

Masoud atakaa katika benchi la Simba kwa mara ya kwanza baada ya kuogopa kufanya hivyo katika mechi iliyopita ambayo timu yake ilishinda 4-0.

Kocha huyo alihofia kukaa kutokana na suaa la vibali vya kufanya kazi na kulikuwa na taarifa Idara ya Uhamiaji walikuwa wanamsubiri kwa hamu.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kila kitu kinashughulikiwa na leo au kesho.

"Mambo sasa ni uhakika, atakuwa katika benchi dhidi ya Yanga akisaidiaa na Kocha Omog," kilieleza chanzo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic