October 27, 2017



Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa, juzi imezindua rasmi Kampeni ya Shinda na SportPesa itakayodumu kwa siku 100 kwa kila mshindi kujishindia bajaji aina ya TVS King. 

Promosheni hiyo, ilizunduliwa juzi kwenye Viwanja vya Manzese, Bakhresa jijini Dar, saa tatu asubuhi.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa promosheni, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema promosheni hiyo ina lengo la kubadili maisha ya Watanzania kiuchumi.

Tarimba alisema: “Sisi kama kampuni tumeona umuhimu wa kuja na promosheni hii ili kuweza kuwainua wateja wetu kiuchumi na kuongezea mianya ya kujipatia kipato zaidi.

“Kama ulikuwa na TVS King moja, basi tunakuongezea ya pili ili uongeze kipato zaidi na kama ulikuwa huna kabisa basi tunakupa hii moja ili uanze leo.

“Promosheni hii itawahusu wale wateja wa SportPesa pekee na kila siku kutakuwa na mshindi, hivyo watakaopata fursa ya kushinda ni wale watakaokuwa wakicheza SportPesa.”

Kuhusu ushiriki Tarimba, alisema: “Kwanza ni lazima tukumbuke kuwa kila siku kutakuwa na mshindi. Kama bado hujawahi kucheza na SportPesa basi hakikisha unajisajili kwa kutuma neno GAME kwenda 15888 na baada ya hapo utatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz kuweka utabiri wako mara nyingi zaidi ili uweze kuingia kwenye droo.” 


Aidha, kutakuwa na zawadi nyingine zinazoshindaniwa ambazo ni pamoja na tiketi tatu kwenda nchini Uingereza kutazama mechi ya EPL, tiketi moja ikitolewa kila mwezi sambamba na jezi orijino zitakazotolewa kila wiki. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic