October 3, 2017




Mwanamichezo maarufu nchini, Mohamed Dewji maarufu kama MO ametoa maoni yake kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na kukemea mashabiki kuingia uwanjani wakati wakishangilia bao katika moja ya mechi za michuano ya Ndondo Cup.

Dewji ameweka video inayoonyesha timu ya Misosi FC ikipata bao la kusawazisha dhidi ya Gongo la Mboto na baada ya hapo mashabiki wa Misosi wanaingia uwanjani kushangilia.

Jambo hilo, limeonekana kumkera MO ambaye anasema ni vizuri kuheshimu sheria za mchezo wa soka ili kusaidia maendeleo ya mchezo huo.


Baada ya maoni yake hayo, wafuatuliaji wa ukurasa wake mbalimbali wameonyesha nao kukerwa na kilichotokea wakiunga mkono kwamba ni vema kufuata sheria na pia kuangalia usalama wa wachezaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic