October 2, 2017




Nahodha wa Simba, Method Mwanjale amesema kikosi chake kina anafasi ya kujiimarisha zaidi na kuzitumia nafasi wanazozipata.

Mwanjale raia wa Zimbabwe amesema wana nafasi ya kufanya vizuri kwa kufunga mabao mengi kama watazitumia nafasi wanazopata.

“Tumetengeneza nafasi lakini haatukuzitumia, lazima tuzitumie ili kupata mabao na kupata ushindi,” alisema.

“Kila mmoja anajitahidi kati yetu, wakati mwingine mambo yanakuwa magumu lakini tunaweza kufanya vizuri zaidi.”

Simba ilipata nafasi nyingi zaidi wakati ikiivaa Stand Unoted kwenye Uwanja wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga, lakini haikuzitumia.


Licha ya kushinda kwa mabao 2-1 lakini Simba ingeweza kushinda mabao mengi zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic