October 17, 2017




Kipa Said Mohamed wa Simba amerejea nchini akitokea nchini India ambako alifanyiwa upasuaji wa goti.

Said maarufu kama Nduda amerejea nchini na kupewa mapumziko ya wiki nane.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema upasuaji wake umekuwa na mafanikio makubwa.

"Lakini amepewa mapumziko hayo na ataendelea kuwa katika usimamizi wa madaktari ili kuangalia maendeleo yake," alisema.

Nduda aliyeibuka kipa bora wa michuano ya Cosafa baada ya kuidakia Taifa Stars mechi moja, amejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic