October 10, 2017


Kiungo mchezeshaji wa Simba, Haruna Niyonzima ameamua kuongeza nguvu zaidi.

Niyonzima raia wa Rwanda amerejea gym ili kujiweka vizuri zaidi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi zijazo ukiwemo ule dhidi ya Yanga, Oktoba 26.

Taarifa zinaeleza Niyonzima ameamua kufanya mazoezi ya ziada kwa kuwa hakuwa na kipindi kizuri wakati wa pre season.

“Alikuwa katika kozi ya ukocha kwao Rwanda kama unakumbuka kile kipindi cha usajili.


“Sasa anaona anahitaji mazoezi ya ziada kuhakikisha anakuwa fiti hasa,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic