October 12, 2017



Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima amesema bado ana jezi za Yanga ambazo amezihifadhi kama kumbukumbu.

Akizungumza na kipindi maarufu cha michezo cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na runinga ya mtandaoni ya Global TV Online, Niyonzima amesema Yanga ni sehemu ya kumbukumbu yake ya maisha ya soka, ndiyo maana anahifadhi jezi hizo.

“Yanga ni sehemu ya maisha yangu ya soka, kuna ubaya gani kwangu kuwa na jezi za Yanga kama kumbukumbu.



“Unajua Yanga ni klabu niliyocheza muda mrefu zaidi kuliko nyingine hadi sasa. Najua sasa niko Simba, ndiyo sehemu ya kazi yangu na ninaiheshimu na kuipenda sana.


“Lakini kubaki na kumbukumbu ya Yanga haina ubaya. Hata kama nitaondoka Simba, pia nitahifadhi jezi za Simba kama kumbukumbu,” anasema Niyonzima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic