October 26, 2017



Kocha wa zamani wa Serengeti Boys, Bakari Shime ambaye sasa anainoa JKT Ruvu amefunguka na kusema Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu sana.

Shime  amesema ligi hiyo ni ngumu sana tofauti na watu wengi wanavyofikiria.

Amesema kuwa, michuano ya Ligi Daraja la Kwanza ni migumu, lakini wanaendelea kupambana kuhakikisha wanapanda daraja na kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.

“Kila timu inayocheza daraja la kwanza inataka kwenda Ligi Kuu Bara. Ajabu kabisa hakuna timu inayofikiria ubingwa.

"Hii inaifanya ligi hii kuwa ngumu sana, tunachofanya ni kuhakikisha tunaendelea kupambana," alisema.

JKT Ruvu kwa sasa ndiyo vinara wa Kundi A wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano lakini Shime anaamini kazi haijaisha na wanataka kupambana zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic