October 21, 2017



Ukubwa wa kikosi cha Simba unaonekana kumpa jeuri Kocha Joseph Omog.

Omog atamkosa John Bocco kama chaguo namba moja katika ushambulizi. Lakini tayari amekamilisha mipango yake ya kumpa nafasi Laudit Mavugo ambaye ataanza katika mechi ya leo dhidi ya Njombe kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mavugo ataanza katika nafasi ya Bocco na ndiye alimchezesha kama mshambulizi namba moja katika mazoezi ya mwisho jana kwenye Viwanja vya Gymkhana.

Lakini Juuko Murshid naye alikuwa pacha wa Method Mwanjale, maana yake ataendelea kusimama katika namba ambayo Salim Mbonde alicheza hadi alipoumia.


Viwango vya wachezaji wanaowaridhi wenzao wanaonekana nao kuwa na kiwango kisichotofautiana na wale ambao watakuwa majeruhi kama Mbonde na Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic