October 12, 2017


Mshambuliaji nyota wa zamani wa AC Milan, George Weah anaelezwa kushinda uchaguzi wa Liberia.

Taarifa zinazosambaa mitandaoni zinaeleza Weah ,51, ameshinda uchaguzi huo wa Urais wa Liberia dhidi ya Rais wa sasa Liberia, Ellen Johnson.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa za kutatanisha ikielezwa bado kuna marimba bado majibu hayajatolewa.

Hivyo watu wametakiwa kusubiri hadi tume ya uchaguzi itakapotangaza.

Weah ni Mwafrika pekee kuwahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wakati akiitumikia AC Milan ya Italia.

Baadaye alijiunga na Manchester City pia Chelsea zote za nchini England. Pia amewahi kuzichezea PSG na Marseille za Ufaransa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic