November 18, 2017




Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
StarTimes waleta kifurushi kipya katika uzinduzi wa JTV
Dar es Salaam 16  Novemba, 2017.
Katika hafla ya uzinduzi wa Jason’s TV, kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yao ya StarTimes walitumia fursa hiyo pia kutangaza kifurushi kipya cha UHURU kwa wateja wake wa antenna.
Kwa wateja wapya na wateja wa siku zote kifurushi hiki kinakuwa kama zawadi kwao kwa kuchagua kutumia king’amuzi cha StarTimes, na hivyo watapata huduma ya kiwango bora kabisa. Akiongea katika hafla hiyo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Juma Suluhu alisema, “Imekuwa ni shauku yetu siku zote kutoa huduma ya kiwango bora kwa Watanzania na kwa gharama nafuu kabisa, kifurushi kipya cha UHURU ni ushahidi tosha na tuna hamu ya kuona wateja wetu pendwa wakikitumia na kufurahia huduma hii.”

Kifurushi kipya cha UHURU kinakuja na chaneli zaidi ambazo awali zilikuwa katika kifurushi cha KILI (kifurushi cha juu zaidi), na kwamba sasa wateja watafurahia chaneli nyingi zaidi kwa bei ile ile. Gharama ya kifurushi cha UHURU ni Tsh 24,000 na kwa kujiunga na kifurushi hiki mteja atapata chaneli saba za ziada kutoka kifurushi cha KILI.
“Chaneli mpya kwenye kifurusi cha UHURU ni pamoja na ST Movie Plus ambayo inaonyesha filamu mpya kutoka Hollywood, FOX yenye tamthiliya za kuvutia kama vile Empire, National Geographic Channel (Nat Geo E) kwa makala maridhawa za kimaisha pamoja na wanyama pori, kwa wapenda michezo tunawaletea ST Sports Premium na ST World Football ambapo watatizama michezo muda wote.

"Pia tunawaletea Star Plus chaneli ya kihindi inayoonyesha filamu na tamthiliya Mpya za Kihindi muda wote, na hatujawasahau watoto kwani tunajua msimu wa msikukuu ni muhimu sana kwao, tunawapatia chaneli ya BABY TV ambayo wataangali  michezo na mazoezi mbalimbali” alisema Juma maarufu kama Sharobaro.

“Tumejitolea kuwaletea huduma bora na kiwango cha juu kabisa, na maono yetu ni kuhakikisha kila familia ya kitanzania inafurahia huduma za kidigitali na maisha ya kidigitali, hivyo kila tunachofanya ni kujaribu kutusogeza katika lengo letu hilo na kifurushi kipya cha UHURU ni hatua kubwa sana.” aliongeza.

Kifurushi kipya cha UHURU kitaanza kufanya kazi tangu tar 17 Novemba mwaka huu. Na kwa wateja wa StarTimes hii ni nafasi ya kipekee ya wao kujiunga na kufurahia huduma hii katika kipindi hiki cha sikukuu.

Huku mashindano makubwa ya Soka yakikaribia na StarTimes tayari imeshapata haki mmiliki ya kurusha matangazo ya moja kwa moja hivyo ni wakati muafaka kwa wateja kujiunga na familia ya StarTimes inayoendelea kukua kila siku ili waweze kufurahia huduma safi na picha za kiwango bora kwa gharama nafuu. 


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic