November 4, 2017




FULL TIME..
DAKIKA 6 ZA NYONGEZA
Dk 89, kona maridadi ya Ajibu, Singida nao kupitia Batambuze wanaokoa vizuri
Dk 89 Yanga wanapata kona nyingine hii ikiwa ni ya pili, inachongwa na Ajibu


SUB dk 88, Yanga wanamtoa Pato Ngonyani na nafasi yake inachukuliwa na Raphael Daud, maana yake, Tshishimbi anarudi namba 6 kuimarisha ulinzi na Daud atakaa juu kuendesha timu
Dk 86, kipa Rostande akiwa chini anatibiwa pia beki Vicent pia
Dk 84 sasa, kidogo Yanga wanaonekana kuanza kupandisha mashambulizi ingawa Mudathir Yahaya anaonekana kuwa kizingiti kwao katika eneo la kati
DK 81 Singida wanamtoa Usengimana na nafasi yake inachukuliwa na Atupele Greeen
Dk 80, krosi safi ndani ya lango la Yanga, wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini goal kick


Dk 78, Singida wanaonekana kuuthibiti mpira zaidi hasa katikati ya uwanja
Dk 75, krosi nzuri ya Makasi, Rostande anatoka vizuri na kuokoa. Sasa kipa huyo na Kutinyu wako chini wakitibiwa
Dk 73,Gadiel yuko chini pale akitibiwa baada ya kuumia na nje anaonekana Mwinyi Haji akipasha
Dk 71 Singida wamepata kona hapa, inachongwa na Batambuse, Yanga wanaokoa vizuri 
SUB Dk 70 Roland Msonjo ameingia upande wa Singida kuchukua nafasi ya Salum Kipaga ambaye ameumia
Dk 68 mchezaji mmoja wa Singida United yuko chini akitibiwa, mguu wa Martin ulimgonga kichwani wakati wakiwania mpia


KADI Dk 64 Chirwa analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha ndani ya eneo la hatari la Singida
SUB Dk 63 JKaseke anakwenda nje anaingia Katsavairo Michelle kuchukua nafasi yake. Huyu tayari ana mabao mawili 
Dk 62 pasi nzuri ya Ajibu, Martin anaingia vizuri kabisa lakini Manyika anawahi kuudaka
Dk 60 Gadieil anaingia vizuri kabisa hapa, anaachia krosi hapa lakini inaishia mikononi mwa Manyika
SUB Dk 59, Yanga wanamtoa Mwashiuya na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 54 mpira wa kona wa Singida United, unagonga nje ya nyavu, lakini wachezaji wa Singida wanamzonga mwamuzini Emmanuel wakilazimisha kuwa ni bao. Inaonekana nyavu zimechanika wakati mpira unagonga nyavu, uliingia kutokea nje


Dk 53 mpira umesimama na wachezaji wanazozana hapa, Yondani akilalamika kutemewa mate
Dk 51 Usengimana anaingia vizuri kabisa hapa, Vicent anaokoa na kuwa kona
Dk 50 Rusheshangoga anaachia mkwaju, Yanga wanaokoa ni kona. Inachongwa na Makasi lakini hakuna mtu hapa
Dk 49, Singida wanashambulia tena hapa, mara nyingine Kaseke anaangushwa
KADI Dk 46 kadi ya kwanza ya njano inakwenda kwa Kaseke, mwamuzi akisema amejiangusha. Yuko chini anatibiwa pale
Dk 46 faulo nzuri ya Makasi, kipa Rostande anaokoa vizuri kapa
Dk 45, kipindi cha pili kimeanza kwa kazi na Singida wanakuwa wa kwanza kuingia kwenye lango la Yanga inakuwa faulo

MAPUMZIKO
-Rusheshangoga analala vizuri kabisa kumzuia Mwashiuya aliyekwua anaambaa ambaa pembeni


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45 sasa, kila timu inajitahi kutaka kupata bao la kipindi cha kwanza
Dk 43 Kutinyu anaachia mkwaju mkali kabisa, unamkuta kipa Rostande anaokoa vizuri kabisa
Dk 42, nye ya lango la Yanga, Kaseke anaachia mkwaju mkali kabisa lakini linaokolewa
Dk 40 Chirwa anamtoka beki wa kulia wa Singida, lakini krosi yake inakuwa kuubwa inaokolewa
Dk 39 pasi nyingine nzuri inamfikia Mwashiuya lakini mwamuzi Emmanuel Mwandembwa anasema alikuwa ameotea
Dk 35 Yanga wanapata kona inachongwa lakini Singida wanaokoa kwa ulaini
Dk 34, United wanaingia vizuri tena katika lango la Yanga lakini mpira wa mwisho wa Kiggi Makasi unakuwa dhaifu
Dk 32, Usengimana na Yondani wanaonyeshana kazi hapa, mwamuzi anasema Yondani amecheza kindava
Dk 29 sasa, mpira kidogo unaonekana kupoteza kasi na ile mipango madhubuti na kila timu inacheza ikiwa imetanguliza tahadhari kubwa


Dk 25, Ajibu anapiga faulo maridadi kabisa lakini Salum anaokoa mpira
Dk 22 pasi safi ya Ajibu, Mwashiuya anatanguliwa lakini beki Lusheshangoga anamuangusha hapa nje kidogo ya lango la Singida
Dk 21, Kaseke mara nyingine anaingia hapa ndani ya 18 ya Yanga lakini Pato nawahi na mpira unafika mkononi mwa kipa Rostande
Dk 21, Usengimana alikuwa akimlalamikia mwamuzi kuhusiana na Yondani kumkanyaga
Dk 20, Kaseke anaingia vizuri kabisa lakini pasi yake ya mwisho inaishia mikononi mwa Vicent
Dk 18, Singida wanafanya shambulizi jingine zuri lakini Yondani anamthibiti vizuri Usengimana, mpira unatoka na kuwa goal kick


Dk 16 shuti kali la kwanza linapigwa na Kutinyu lakini kipa Rostande wa Yanga analala na kudaka kwa umaridadi kabisa
Dk 14, Yanga wanapoteza nafasi nzuri baada ya kipa Manyika kuokoa na lango likabaki halina mtu, lakini Mwashiya akapiga shuti dhaifu ambalo halikulenga lango
Dk 12, Ajibu anapiga mkwaju wa faulo lakini unatoka juu ya lango la Singida
Dk 11, Mashiuya anawachambua mabeki wa United na Kaseke analazimika kumuangusha, inakuwa faulo
Dk 10 sasa, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja huku kukiwa na mashambulizi ya rasharasha kutoka kila upande na mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja


Dk 7 Yanga walikuwa wanagongeana vizuri karibu na lango la Singida, Tshishimbi anawekwa chini, faulo
Dk 5, pasi nzuri ya Kutinyu, Youthe Rostand Jehu anatokea na kuuwahi vizuri kabisa
Dk 4, Ajibu anaingiza majaro nzuri kabisa karibu na lango la Singida lakini shuti la chirwa linatoka nje na kuwa goal kick
Dk 1 Mechi inaonekana kuanza kwa kasi, Yanga wanajibu mashambulizi na Singida wanatoa na mpira unakuwa wa kurushwa pia

Dk 1, Singida United wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga, Yondani anatoa na kuwa wa kurushwa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic