November 11, 2017


Kiungo Said Hamis Ndemla anatarajia kuanza majaribio katika klabu ya AFC, keshokutwa Jumatatu.

Ndemla tayari yuko jijini Stockholm jijini Sweden akijiandaa na kuanza majaribio na timu hiyo imetoa siku 14.

“Bado mechi mbili za ligi, AFC imekuwa ikipambana kubaki Ligi Kuu Sweden. Lakini Ndemla ameishapata nafasi ya majaribio na ataungana na wenzake Jumatatu,” kilieleza chanzo kutoka Sweden.

Ndemla ameondoka nchini juzi baada ya kuitumikia Simba katika mechi dhidi ya Mbeya City mjini Mbeya.


2 COMMENTS:

  1. Hiyo timu inapambana kurudi ligi kuu. Ilishuka mwaka jana mzee baba.

    ReplyDelete
  2. Nipo Sweden Saleh. Rekebisha habari yako.AFC imeshashuka daraja.Imecheza mechi 30.Imeshinda 4 sare 8 na kufungwa 18.Imefunga magoli 28 na kufungwa 55.Imeteremka pamoja na Halmstad. Lea sasa sio timu yenye mwelekeo mzuri kutokana na matatizo ya uongozi na uchumi. Huenda wachezaji wengi wakaondoka.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic