November 11, 2017



Uongozi wa Yanga umesema unataka wachezaji wanaojituma na wenye nia ya kuisaidia klabu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesisitiza kwamba wale wachezaji wanaotanguliza fedha badala ya kupambana kwa ajili ya klabu hawatakuwa na nafasi.


“Atakayeleta sintofahamu atachukuliwa hatua. Sisi
tunahitaji mchezaji ambaye amelenga kuisaidia klabu,” alisema.

“Kama lengo lake litakuwa ni fedha pekee na anapanga kutuvuruga basi tutaachana naye.


“Lakini nasisitiza, tunahitaji wacheaji walio fiti ambao watakisaidia kikosi chetu. Kama tutaona mchezaji ni majeruhi kwa muda mrefu tutaachana naye.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic