November 9, 2017




Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku kikiongeza baadhi ya wachezaji wao wa U20.

Hiyo ni baada ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake takribani kumi na kati ya hao wapo waliokuwepo kwenye timu ya Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin.

Tofauti na wachezaji hao, wapo wengine ni majeruhi wapo nje ya uwanja wakkisumbuliwa na majeraha mbalimbali na kati ya hao ni Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe.


Timu hiyo, imeendelea katika mazoezi ya leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam chini ya kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa na Noel Mkandila.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic