Gazeti namba moja la michezo nchini, lmedhamini michuano ya soka ya ufukweni ya vyuo.
Michuano hiyo inaendelea katika ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.
Timu 16 zinashiriki michuano hiyo ya Beach Soccer ambayo imeanza leo na itaendelea kesho Jumapili.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ambao ni wachapishaji wa gazeti la Championi amesema lengo lao ni kusaidia michezo.
“Sisi tumejitokeza kuonyesha tunaunga mkono michezo. Lengo Kuu ni kusaidia na kuwasisitiza watu michezo ni muhimu kwa afya na ajira,” alisema.
Ally maarufu kama Jembe, amewaomba watu kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment