November 23, 2017


Kwa mwonekano, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina ni mtaratibu sana na wengi hujiuliza anaweza vipi kuwa kocha mzuri.

Lakini baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, wengi wakaanza kumuamini.

Pamoja na hivyo, inakuwa vigumu kuamini kwa umbo lake kubwa anaweza kuwa akifanya mazoezi kwa mifano.

Lwandamina ameonyesha yuko fiti katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika juzi baada ya kufanya mazoezi kwa vitendo huku akiruka juu kama Mmasai anapokuwa akicheza ngoma.

Kocha huyo raia wa Zambia alimaliza kabisa baada ya kuamua kutoa ,mfano katika upigaji wa push up wakati akiwaonyesha wachezaji wake.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic