November 2, 2017



MICHUANO ya Afrika Mashariki na kati Cecafa baada ya kusimama kwa muda mrefu sasa imerudi tena huku timu za taifa ya Tanzania zimechaguliwa kushiriki michuano hiyo yatakayoanza Novemba 25 hadi 9 Desemba nchini Kenya.

Akizungumza na Waandishi wa Habari , kwenye Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kaimu Katibu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidau alisema kuwa timu za taifa za Tanzania kuanzia ya wakubwa hadi chini ya miaka 20 hadi 17 zinatarajia kujanda na michuano ya Cecafa Challenge Cup nchini Rwanda.


“Timu yetu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kujianda kwenda kushiriki michuano Cecafa Challenge Cup ambayo yataanza Novemba 25 hadi 9 Desemba.

“Ni mashindano ambayo yalitakiwa yafanyike miaka miwili iliyopita ikwa ni jitihada za kurudisha mashindano ya Cecafa kama ilivyokuwa zamani lakini pia Tanzania tumechaguliwa kuanda michuano hii ya Cecafa chini ya miaka 17 mwakani,”alisema Kidao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic