November 27, 2017


Wakati tetesi za kutemwa kwa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo, kiungo mchezeshaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kukosa timu kama akiachwa.

Mavugo ni kati ya wachezaji waliopo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo la msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwa kile kinachotajwa kiwango chake kushuka.

Mrundi huyo, tayari ameanza kunyatiwa na baadhi ya klabu za nje ya nchi na kati ya hizo ni Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema Mavugo bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, lakini vitu vidogo ndiyo vinamfanya ashindwe kutimiza majukumu yake.

Niyonzima alisema, mshambuliaji huyo kinachomfanya ashindwe kucheza ni presha kubwa iliyopo kwenye timu huku akimtabiria kuwa akienda kwingine atacheza vizuri.

“Mavugo siyo mbaya kiasi hicho, binafsi naona ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika timu.

“Lakini kitu kikubwa kinachomfanya ashindwe kucheza vizuri ni presha iliyopo katika timu pekee na siyo kitu kingine.

“Ninakuhakikishia akienda timu nyingine tofauti na Simba atakuwa tegemeo, kwani ana uwezo mkubwa,” alisema Niyonzima.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Niyonzima mwenyewe aache kucheza kwa presha. Jana ametukosesha goli mbili za wazi dhidi ya lipuli endepo angetulia na kutokuwa na presha. Ni mchezaji mzuri ningepata muda wa kuzungumza nae ningemuomba akifika ndani ya 18 anapaswa kutulia na kutumia akili kuliko kupaparika.Halafu awe anafanya maamuzi sahihi kwa muda muafaka,mara kadhaa kanyang'anywa mpira mguuni kwa sababu ya kuchelewa kutoa maamuzi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic