November 27, 2017

Kocha Mkuu wa Dodoma FC ya mkoani Dodoma, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amemvaa beki wa Yanga, Kelvin Yondani kwa kusema kuwa, licha ya yeye kuwa ndiye aliyemuibua lakini amekuwa akimchunia kwa kutompa salamu.

Yondani ambaye alitokea Simba misimu kadhaa iliyopita, amekuwa akionyesha kiwango cha hali ya juu katika timu yake ya Yanga.

Julio ambaye kwa sasa anaitumikia Dodoma FC, amekuwa akisifika kwa kuwatumia wachezaji wakongwe katika timu anazofundisha za daraja la kwanza, ikiwemo Mwadui FC aliyoipandisha misimu mitatu iliyopita.
Julio
Akizungumza na Championi Jumatatu, Julio alisema kuwa, amekuwa miongoni mwa makocha ambao wameibua wachezaji wengi wanaofanya vyema kwenye ligi akiwemo Yondani lakini wamekuwa hawampi hata salamu licha ya kuwaibua.

“Nahitaji kufanya usajili mzuri katika timu yangu najua hapa Tanzania kuna wachezaji wengi wazuri lakini watu hawaelewi tu, kuna sehemu mbalimbali naangalia wachezaji kwa ajili ya kuwasajili katika usajili wa dirisha dogo.
Yondani

“Mimi ni kocha ambaye nawajua vyema wachezaji wazuri, kwani kuna wachezaji wengi ambao nimewaibua akiwemo Yondani na Henry Joseph na wengineo wengi ambao walikuwa hawajulikani, nimewaibua na kuweza kutambulika kwenye soka kutokana na uwezo waliouonyesha na kuwa tegemeo.

“Cha kushangaza Yondani hata meseji hajawahi kunitumia wala kunisalimia, lakini kwa upande wangu mimi ni kocha, naendelea kuibua vipaji vya wachezaji tofautitofauti,” alisema Julio.


CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic