November 27, 2017

Shirikisho la Kimataifa la Soka la Kimataifa (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 katika msimu wa mshindano mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni Mfaume Ali, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina Zablon.

Waamuzi Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli, Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na kwa wanawake Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace Wamala.

Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni  Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic