November 12, 2017



Mshambuliaji Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma anatarajia kurejea nchini kesho.

Taarifa kutoka Yanga zinaeleza Ngoma atarejea na kujiunga na wenzake baada ya kupata matibabu nchini mwake.

"Tumeambiwa anakuja kesho lakini kama utazungumza na Meneja Hafidh au Katibu Mkwasa watakuwa wanajua anakuja lini.

"Lakini inaweza isiwe na uhakika sana kwa kuwa hata wakati wa kuondoka mwisho alimuaga kocha na kocha sasa hayupo, huenda naye atakuja kesho," kilieleza chanzo.

Ngoma aliamua kwenda kupata matibabu nchini Zimbabwe.

Wiki iliyopita, picha kadhaa zilimuonyesha Ngoma akiwa ameanza kujifua gym huko Zimbabwe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic