November 28, 2017




Kikosi cha Manchester United kimeshawasili Watford kwa ajili ya mchezo wao wa leo dhidi ya Watford utakaopigwa kwenye Uwanja wa Vicarage Road ikiwa ni muendelezo wa Premier League.

Kikosi hicho kiliongozwa na kocha wao, Jose Mourinho ambaye alionekana kuwa mstari wa mbele katika kiuto cha treni cha Stockport kabla ya kuanza kwa safari hiyo ya saa mbili na nusu kutoka Manchester kuelekea London.  

Msafara huo pia ulikuwa na mkongwe Zlatan Ibrahimovic pamoja na mchezaji aliyesajiliwa kwa bei kubwa kuliko wote klabuni hapo, Paul Pogba. Ushindi pekee ndiyo utakaowafanya wapunguzo tofauti ya pointi kati yao na vinara wa ligi hiyo, Manchester City.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic