Baada ya kumalizana na kikosi cha Polisi Dodoma,Kocha Ali Bushiri anatarajia kuanza kazi hivi karibuni akisaidiana na Jamhuri Kihwelo maarufu kama Julio.
Bushiri anaungana na Julio kuongeza nguvu katika kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Kocha huyo wa zamani wa Mwadui FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara, ataanza kazi ya kukinoa kikosi hicho leo Jumatatu ambapo timu hiyo imepiga kambi katika Chuo cha Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Frank Geofrey, amesema kila kitu kimekamilika na Bushiri yuko tayari kuanza kazi.
"Pamoja na Bushiri, upande wa makipa tumemchukua kocha wa makipa, Mohammed Silima kutoka Polisi Zanzibar ambapo awali hawakuwa na kocha wa makipa," alisema.
Polisi Tanzania ni kati ya timu zinazofanya vizuri katika Ligi Daraja la Kwanza na matumaini ya kurejea Ligi Kuu Bara,
Kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye Kundi B ikiwa na pointi16 katika mechi tisa ilizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment