Manchester United imefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya kuibaa CSKA Moscow ya Russia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mechi hiyo itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.
Beki Phill Jones amerejea na huenda Kocha Jose Mourinho anaweza kumtumia katika mechi hiyo wakitaka kushinda baada ya kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Basle ya Uswiss.
Katika mechi ya kwanza dhidi ya CSKA, Man United ikiwa genii ilishinda kwa mabao 4-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment