December 30, 2017





Unakumbuka mara ngapi umewahi kuwa na marafiki wakakuangusha, lakini wapo marafiki ni zaidi ya ndugu kutokana na unavyoishi nao?

Lakini umewahi kujiuliza wewe, kwamba mara ngapi umewaonyesha upendo au kuwalipa upendo wa chini ya moyo wako marafiki waliokujali.

Rafiki ni ndugu au zaidi hasa anapokuwa mwema kwako na mapenzi yake huwa makali, maradufu ya wale unaoamini ni ndugu zako.

Nitatumia mfano huu wa mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid na na timu ya taifa ya Ureno.

Kwanza nianze kumpongeza aliyetafsiri na mimi licha ya kuwa nimesoma na kuvimaliza vitabu vitatu vya maisha ya Ronaldo kutoka Madeira, Ureno, mfano huu, unaweza kukufunza mengi sana. HAYA TWENDE SASA.

Ronaldo alipopokea tu tuzo zake hivi karibuni, Ronaldo alisema ... Shukrani zimwendee Alberto Fantrau. Kisha akasema: "Naam mimi ni mchezaji bora na mafanikio yangu yote yamesababishwa na rafiki yangu Alberto"
Watu walitazama na kusema, "Huyu Fantrau ni nani?" Kisha Ronaldo aliendelea kusema: "Tulicheza pamoja katika timu ya vijana.Watu wa sporting Lisbon walikuja kutazama, walituambia kuwa mshambuliaji ambaye angefunga magoli mengi zaidi watamchukua.

Siku hiyo tulishinda 3-0. Nilifunga bao la kwanza na kisha Albert alifunga 2 kwa kichwa. Na kisha bao la 3 lilikuwa lililovutia kila mtu. Alberto alianza kutokea kwa pembeni, kisha akajikuta uso kwa uso na kipa, alimpunguza kipa na kujikuta yeye na bao tu kiasi kwamba ilikuwa auskume tu golini mpira. Wakati huo nilikuwa nakimbilia upande wake. Na badala ya kufunga , Alberto aliamua kunipasia mpira na mimi nikafunga. Hivi ndivyo nilivyojikuta katika Sporting Lisbon Academy. Baada ya mchezo nilikwenda kwake, nikamwuliza "kwa nini ulifanya hivyo?" Naye akajibu, "Kwa sababu najua kwamba wewe ni bora kuliko mimi"

Waandishi Walipenda kujua zaidi, walianza kuchunguza na waliweza kukutana na Alberto Fantrau kumwuliza kama hadithi waliyoambiwa na Ronaldo ni kweli, na aliihakikishia, akiongeza kuwa kazi yake kama mchezaji wa mpira wa miguu ilimalizika baada ya mechi ile wakati ilikuwa nafas ya pekee kuwa mchezaji mahiri kama angeajiriwa na FC Sporting Lisbon. Badala yake amejikuta akibaki mtaani bila ajira.

Hata hivyo, waandishi wa habari, waliangalia nyumba yake ya kifahari na Mercedes benz anazomiliki wakamuuliza Alberto," huna ajira yoyote je ni jinsi gani unaweza kuwa na nyumba na gari la kifahari? Hauonekani kuwa na kipato cha kumiliki hivi vitu" jibu la Alberto: "Hiyo yote? ni Ronaldo

Maadili ya hadithi hii:
Huu ni wakati mzuri kwako kujipima au kujiuliza kama kweli umewahi kufanya jambo kama la Ronaldo kwa kipimo chako au kuna rafiki amewahi kukufanyia hivyo.


Ronaldo na Alberto watakuwa wamekufunza jambo na lazima ujue kusamehe na kujali ni jambo unalohitaji kufanyiwa na ukumbe pia unahitaji kuwafanyia watu na hutajua malipo yake. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic