December 30, 2017


Simba kwa mara ya kwanza chini ya Kocha Masoud Djuma imetangaza kikosi chake ambacho kitaivaa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kikosi hicho kinaonyesha Shiza Kichuya akiwa namba tatu, hambo ambalo limeonekana kuwachanganya sana mashabiki.

Hata hivyo, Kocha Djuma ametumia mfumo huo ambao huwachanganya wapinzani kisaikolojia kwa kutegemea uchezaji tofauti lakini kutengeneza hali ya sintofahamu dakika chache kabla ya mechi.

Lakini kama utakiangalia vizuri kikosi hicho utaona hakika tofauti na vikosi vingine na huenda ni katika karatasi tu lakini katika hali ya kawaida, Kichuya anarejea kucheza namba yake ambayo ni saba au wingi ya kulia. Inakuaje?

Manula atapaki langoni, Bukaba ni namba mbilina tatu anakwenda kucheza Nyoni ambaye katika kikosi anaonekana ni namba tano, namba ambayo itachezwa na James Kotei ambaye anashirikiana na Juuko Murshid aliye namba nne.

Kwa kuwa Kotei hayupo namba nane, namba hiyo ataitumikia Muzamiru ambaye katika kikosi anaonekana ni namna 10, jambo ambalo si sahihi na utaona katika ushambulizi mbele kutabaki hivi, saba ni Kichuya, nane ni Muzamiru, tisa ni Bocco ambaye katika kikosi anaonekana ni namba sana, kumi ni Liuzio na 11 ni Mo Ibrahim.

Hiki ndiyo kikosi cha kwenye karatasi....


1.Aishi Manula - 28
2.Paul Bukaba - 23
3.Shiza Kichuya - 25
4.Juuko Murshid -06
5.Erasto Nyoni - 18
6.Jonas Mkude - 20
7.John Bocco - 22
8.James Kotei -03
9.Juma Luizio - 10
10.Mzamiru Yassin - 19
11.Mohamed Ibrahim -4

SUBS.
1. Emanuel Mseja - 30
2.Mohamed Hussein - 15
3.Yusufu Mlipili - 05
4. Said Hamisi - 13
5.Jamali Mwambeleko-26
6.Nicholas Gyan - 29.

7.Moses Kitandu - 35.


 Lakini kama utakipanga sahihi kitakavyocheza itakuwa hivi....

1. Aishi Manula - 28
2. Paul Bukaba - 23
3. Erasto Nyoni - 18
4. Juuko Murshid -06
5. James Kotei -03
6. Jonas Mkude - 20
7. Shiza Kichuya - 25
8. Muzamiru Yassin - 19
9. John Bocco - 22
10. Juma Luizio - 10
11. Mohamed Ibrahim -4


SUBS.
1. Emanuel Mseja - 30
2.Mohamed Hussein - 15
3.Yusufu Mlipili - 05
4. Said Hamisi - 13
5.Jamali Mwambeleko-26
6.Nicholas Gyan - 29.

7.Moses Kitandu - 35.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic