December 30, 2017




Beki mpya wa Simba, Asante Kwasi ameonekana kweli hataki utani na amepania kufanya kweli.

Kwasi anasubiri kikosi cha Simba kirejee kutoka Mtwara ili ajiunge nacho lakini hachoki kufanya mazoezi makali.

Baada ya siku mbili za ufukweni kule Coco, Kwasi jana aliamua kufanya mazoezi katika ngazi za hoteli akipanda na kushuka zaidi ya mara 50.

Beki huyo raia wa Ghana anaonekana yuko fiti na anataka kucheza na kuisaidia Simba ili ajitangaze vizuri.

Kwasi amejiunga na Simba akitokea Lipuli ya Iringa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic