December 30, 2017



Bosi wa benchi la ufundi la Singida United, Hans van Der Pluijm amejipanga kuzipiku Simba na Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kushinda kila mechi iliyo mbele yake akianza na Njombe Mji, kesho Jumapili.


Singida ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 20 nyuma ya Yanga ambayo ina pointi 21, huku Simba ikiongoza kwa kuwa na pointi 23.

Pluijm amesema anaijua Njombe ni moja ya timu nzuri kwenye ligi, lakini amejipanga kuhakikisha anafanikiwa kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri.


“Mechi yetu na Njombe itakuwa ngumu lakini tupo tayari kupambana ili kuweza kufanikiwa kuwa katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi, tunahitaji kujituma ili tuweze kukaa kileleni.


“Tumepitwa pointi chache na Simba na Yanga hivyo nimepanga kupambana tuwe kileleni japokuwa nitawakosa Raphael Kutinyu ambaye ni majeruhi na Juma Kennedy mwenye kadi tatu za njano.


“Ligi ni ngumu na ina ushindani, Njombe ni moja kati ya timu zenye ushindani, lakini nimewaandaa vyema wachezaji wangu kuhakikisha tunashinda,” alisema Pluijm.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic