December 12, 2017



Lipuli wamesisitiza Asante Kwasi bado ni mali yao na si mchezaji wa Simba.

Wakati wanasema hivyo, taarifa zinaeleza Kwasi raia wa Ghana anaendelea mazungumzo na Simba.

Msemaji wa Lipuli, Clement Sanga amesema bado uhamisho haujafanyika na Kwasi ni mali ya Lipuli.

“Kuna wengine wanasema ameishatua Simba, si kweli,” alisema.

Kama Blog hii ilivyoeleza katika stori ya kwanza, bado kuna mazungumzo kati ya Kwasi na Simba na yanaonekana kwenda vizuri.

Hata hivyo, Simba imekuwa ikijiuliza kumsainisha beki katika nafasi ya Method Mwanjale aliyeachwa au mshambuliaji.


Kama uamuzi wa mwisho itakuwa ni beki, basi Kwasi atakuwa na nafasi kubwa ya kujiunga na Simba.

1 COMMENTS:

  1. Wanamng'ang'ania mavugo wa nini wakati ameshindwa kuendana na kasi ya timu?? Mchezaji wa nje bado anapigwa bench na anakumbatiwa wa nn?? Au ni rafiki yake na omog anamlinda wakati simba haifanyi vizuri kwa sababu hakuna mfungaji mahiri. Kama ni hivyo mm kama shabiki wa simba naona bora omog aondoke maana anatuchelewesha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic