Jitihada za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) za kuwasiliana na Mwendeshaji wa mfumo huo waliokasimiwa na Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) walioko Tunis, Tunisia ili kuziwezesha timu kufanya usajili, zimefanikiwa.
Mtandao huo kwa sasa upo wazi. Hivyo TFF inazitaka timu zote sasa kukamilisha usajili kuanzia pale walipokwama. Timu zinatakiwa kusajili kabla ya Desemba 23, mwaka huu.
Desemba 15, mwaka huu mfumo wa usajili kwa njia ya TMS ulifeli hali iliyosababisha vilabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.
Katika mawasiliano na kampuni hiyo, FIFA na CAF wamekuwa wakipewa Taarifa ya kila hatua inayochukuliwa na TFF hadi mfumo huo kufunguka leo Desemba 19, 2017.
Bado TFF inasisitiza vilabu vyote kuzingatia kusajili kwa wakati pale inapotokea dirisha la usajili limefunguliwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment